Shirikisho la Mpira wa Wavu Tanzania (TVF) linawatangazia wanachama na wadau wote wa mpira wa wavu kuhusu uchaguzi mkuu utakaofanyika tarehe 21 Desemba 2025 jijini Dodoma. Nafasi mbalimbali zimetangazwa.
4 min
Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Wavu Tanzania (TVF) inatangaza rasmi kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa TVF utakaofanyika tarehe 21 Desemba 2025, jijini Dodoma.
Nafasi zinazogombewa ni kama ifuatavyo:
- Rais: Nafasi 1
- Makamu wa Rais: Nafasi 1
- Wajumbe wa Bodi (Wanaume): Nafasi 2
- Wajumbe wa Bodi (Wanawake): Nafasi 2
Gharama za Kuchukua Fomu:
- Rais na Makamu wa Rais: TZS 1,000,000
- Wajumbe wa Bodi: TZS 500,000
Fomu:
Fomu na hati nyingine zinapatikana katika link zifuatazo; bonyeza ili kudownload.
👉🏽 Katiba ya TVF [Toleo la 2023]
👉🏽 TVF Electro Regulations 2025
Mwisho wa kurejesha fomu ni Jumatatu, tarehe 24 Novemba 2025 saa 10:00 jioni. Fomu zirejeshwe kupitia barua pepe: uchaguzi@tvf.or.tz
Taarifa za Malipo:
Malipo ya fomu yafanywe kupitia akaunti ifuatayo:
Jina la Akaunti: Tanzania Volleyball Association
Benki: NMB
Namba ya Akaunti: 24510025069
Wakati wa kurejesha fomu, hakikisha umeambatanisha risiti ya malipo (Pay in Slip) kuthibitisha ulipaji wako.
Shirikisho la Mpira wa Wavu Tanzania (TVF) limetangaza kalenda yake kamili ya shughuli za mwaka 2026, ikiwa na zaidi ya mashindano 25 ya kitaifa na kimataifa. Kalenda hiyo inajumuisha Ligi ya Taifa (TVNL), Kombe la Taifa, Bingwa wa Afrika kwa wanawake na wanaume, mashindano ya vijana, na shughuli nyingine zinazoendelea katika miji mbalimbali ikiwemo Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza, na Zanzibar. Pakua kalenda ili usikose tukio lolote la mpira wa wavu mwaka huu.
TVF imetoa matokeo ya uchunguzi wa sifa za wagombea wa uongozi ambapo baadhi wamepitishwa na wengine wamekatwa. Kamati imetoa utaratibu wa pingamizi na rufaa kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi.
Hati mpya kupatikana kwenye tovuti zikiwemo: Kanuni za Ligi na Usajili [2025], Kanuni za Maadili, Kanuni za Uchaguzi, Kanuni za Fedha na Utawala (Machi 2025) na Katiba ya hivi karibuni [Toleo la 2023]