TAVA yaendelea kuboresha sheria na kanuni zinazoongoza mpira wa wavu nchini - ikigusia msimu wa mashindano, mfumo, mahitaji na ada za usajili kwa mwaka 2023.
1 min
Chama cha Mpira wa Wavu Tanzania, TAVA, kimefanya maboresho ya Kanuni za Usajili za Mwaka 2022 Toleo la Mwezi Februari ili kukidhi mahitaji ya wakati. Kwa kuzingatia kanuni hizi, TAVA inalenga kusimamia haki na wajibu wa kila mshiriki huku ikilinda hadhi zao nyakati zote. Utekelezaji na usimamizi wa Sheria, Kanuni na Miongozo utaanzia ngazi ya Timu/ Klabu, Wilaya, Mkoa, Kamisheni husika ambapo ngazi ya Mwisho niofisi ya Sekretarieti ya TAVA.
Pakua nakala ya Kanuni za Ligi na Usajili 2023/24 hapa.
Shirikisho la Mpira wa Wavu Tanzania – TVF, linawataarifu wadau wote kuwa dirisha la usajili kwa Vituo na Shule za kulelea Watoto, Taasisi binafsi, Makocha na Waamuzi limefunguliwa kuanzia leo tarehe 2/2/2024 hadi tarehe 16/2/2024.
Orodha ya Wachezaji Waliochoguliwa Kuwakilisha Timu ya Taifa Katika Mashindano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki 2024
Chama cha Mpira wa Wavu Tanzania (TAVA) kimefungua dirisha la usajili kwa msimu wa mashindano wa 2023/24, kuanzia tarehe 13/11/2023 hadi 12/12/2023. Maboresho ya kanuni yamefanyika kulingana na mahitaji ya wakati, na usajili utahusisha vilabu, makocha, wachezaji, waamuzi, na taasisi nyingine.