TAVA imetangaza ufunguzi wa dirisha la usajili kwa msimu wa mashindano wa 2023/24, likianza tarehe 13/11/2023 hadi 12/12/2023. Mfumo wa usajili umepitia maboresho ya kanuni ili kukidhi mahitaji na unahusisha vilabu, makocha, wachezaji, waamuzi, na taasisi nyingine.
3 min
Chama Cha Mpira wa Wavu Tanzania – TAVA kinawataarifu wadau wote kuwa Dirisha la usajili kwa msimu wa mashindano kwa mwaka 2023/24 unafunguliwa tarehe 13/11/2023 saa moja asubuhi. Mfumo huu wa usajili utakuwa wazi kwa siku thelathini (30) hadi tarehe 12/12/2023 saa sita usiku. Sambamba na kufunguliwa dirisha la usajili, kumefanyika maboresho ya Kanuni za Usajili za Mwaka 2022 Toleo la Mwezi Februari ili kukidhi mahitaji ya wakati. Viongozi na wadau wote wanaelekezwa kuzisoma nakuzielewa kanuni hizo kabla ya kufanya usajili. Mfumo wa usajili utakuwa na mambo yafuatayo;
Kamati kuu ya TAVA inawaomba wenyeviti wa mikoa kuhakikisha taarifa hizi zinawafikia viongozi wote wa Vilabu, Makocha na Waamuzi na kuratibu ama kufuatilia utekelezaji wake ikiwa ni pamoja nakuwasainia viongozi wa vilabu na taasisi barua za utambulisho ili kukamilisha zoezi hili kwa wakati. Hakutakuwa na Klabu, Taasisi, Kitalu wala muhusika yoyote atakayesajiliwa pasipokuwapo na ufahamuwa uongozi wa Mkoa. Kwa changamoto zozote za kimfumo wasiliana na namba zifuatazo: 0764837005 au 0762550211.
Bonyeza anuani ya usajili ya TAVA kuingia kwenye mfumo - https://register.tvf.or.tz/
Shirikisho la Mpira wa Wavu Tanzania – TVF, linawataarifu wadau wote kuwa dirisha la usajili kwa Vituo na Shule za kulelea Watoto, Taasisi binafsi, Makocha na Waamuzi limefunguliwa kuanzia leo tarehe 2/2/2024 hadi tarehe 16/2/2024.
Orodha ya Wachezaji Waliochoguliwa Kuwakilisha Timu ya Taifa Katika Mashindano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki 2024
TAVA yaendelea kuboresha sheria na kanuni zinazoongoza mpira wa wavu nchini - ikigusia msimu wa mashindano, mfumo, mahitaji na ada za usajili kwa mwaka 2023.