Shirikisho la Mpira wa Wavu Tanzania – TVF, linawataarifu wadau wote kuwa dirisha la usajili kwa Vituo na Shule za kulelea Watoto, Taasisi binafsi, Makocha na Waamuzi limefunguliwa kuanzia leo tarehe 2/2/2024 hadi tarehe 16/2/2024.
3 min
Shirikisho la Mpira wa Wavu Tanzania – TVF, linawataarifu wadau wote kuwa dirisha la usajilikwa Vituo na Shule za kulelea Watoto, Taasisi binafsi, Makocha na Waamuzilimefunguliwa kuanzia leo tarehe 2/2/2024 hadi tarehe 16/2/2024.
Hivyo basi, kwa wale ambao walikuwa hawajasajili bado taasisi zao na ambao walikuwa hawajakamilisha taratibu za kusajili watumie dirisha hili kukamilisha zoezo hilo.
Makochana Waamuzi: baadhi ya makocha na waamuzi wamefanikiwa kusajiliwa kikamilifu na wengine walikutana na changamoto mbalimbali katika kusajili wanatakiwa kuingia kwenye mfumo kwa ajili ya kurekebisha taarifa zao na kuna wengine ambao walilipia na hawakufanikiwa kukamilisha usajili nao wanatakiwa kuingia kwenye mfumo kwa ajili ya kukamilisha usajili wao pia ambao hawajasajili kabisa wanatakiwa wajisajili mapema kabla ya muda wa dirisha kufungwa.
Wahusikawote mnasisitizwa kujisajili mapema kwa ajili ya kupata vibali vya kushirikishughuli zote zinazosimamiwa na Shirikisho la Mpira wa Wavu – TVF
Link za usajili
👉🏽 Shule na Vituo vya Kukuza Vipaji
👉🏽 Makocha
👉🏽 Waamuzi
Kwa changamoto zozote za kimfumo na kiufundi wasiliana na namba zifuatazo
+255 764 600 741 – Mkurugenzi wa Ufundi
+255 764 837 005 – Afisa TEHAMA (IT)
Imetolewa na Idara ya Habari na Mawasiliano
Orodha ya Wachezaji Waliochoguliwa Kuwakilisha Timu ya Taifa Katika Mashindano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki 2024
TAVA yaendelea kuboresha sheria na kanuni zinazoongoza mpira wa wavu nchini - ikigusia msimu wa mashindano, mfumo, mahitaji na ada za usajili kwa mwaka 2023.
Chama cha Mpira wa Wavu Tanzania (TAVA) kimefungua dirisha la usajili kwa msimu wa mashindano wa 2023/24, kuanzia tarehe 13/11/2023 hadi 12/12/2023. Maboresho ya kanuni yamefanyika kulingana na mahitaji ya wakati, na usajili utahusisha vilabu, makocha, wachezaji, waamuzi, na taasisi nyingine.